Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Hujjatul-Islam Sayyid Baqir Rouhani, maarufu kwa jina la “Haj Mirza Baqer,” ambaye ni mwana wa marehemu Sayyid Muhammad, mkwe wa Marja wa zama za Qom, Ayatullah Al-Uzma Haj Sayyid Sadiq Qomi, alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri na wenye mali katika mji wa Qom, huku akiwa pia katika wadhifa wa uongozi wa kidini.
Alikuwa na mchango mkubwa katika kufufua na kuendeleza Sunna njema ya waqf (wakfu). Kwa mchango huu wake, mnamo tarehe 19 Esfand mwaka 1322 (kulingana na kalenda ya Shamsi), alitoa sehemu yake ya umiliki wa pamoja wa Karavansara ya Haj Abbas Qoli na Timcheh Kubwa iliyopo katika soko la Qom, pamoja na vipande vinne vya ardhi ya kilimo katika viunga vya sehemu ya kwanza ya Qom, na kuvikabidhi kama wakfu kwa ajili ya kuadhimisha maombolezo ya Imam Husayn (a.s) na Bibi Fatima Zahra (a.s).

Marehemu Haj Mirza Baqer alikuwa na mapenzi na utiifu wa hali ya juu kwa hadhara tukufu ya Imam Abi Abdillah al-Husayn (a.s). Kwa kiwango hiki cha mapenzi, majlisi ya maombolezo na masimulizi ya msiba wa Imam Husayn (a.s) imekuwa ikiandaliwa kwa utukufu mkubwa kila mwaka katika kumi ya mwisho ya mwezi wa Safar. Mkutano huo wa maombolezo, ambao ulianzishwa wakati wa uhai wake, bado unaendelea hadi leo nyumbani kwake, lililoko katika mtaa wa Gozar Ghaleh, mojawapo ya maeneo ya zamani ya Qom, na hupokelewa kwa shauku na maelfu ya waombolezaji wa Husayn (a.s).
Ni vyema kutaja kuwa wakfu aliloliacha baada ya kufariki, ni miongoni mwa maukufu machache huko Qom yaliyosajiliwa kwa nia mahsusi ya kuadhimisha maombolezo ya Fatimiyya, na bado linafanya kazi kikamilifu hadi wakati huu.
Your Comment